GBROS DE VOICE AACHIA NGOMA MPYA IITWAYO "KALE"
Ngoma mpya iendayo kwa jina la "KALE" imekuwa ni nyimbo ya kipekee yenye beat nzuri na mashairi yaliyopangiliwa iliyoimbwa na msanii Gbros De Voice na kutengenezwa chini ya producer Fraga ndani ya Uprising Music Studios . Bongoka BlogSpot ikiwa na team yake ilimtafuta msanii huyo chipukizi baada ya kusikia nyimbo yake yenye ujumbe mzuri na kutaka kujua ni nini kisa cha yeye kutunga nyimbo hiyo. Kutokana na maelezo yaliyopatikana kutoka kwa msanii huyo anaevuma kwa sasa jijini amesema kuwa ameandaa nyimbo hiyo maalum kwa ajili ya kuwakumbusha MABINTI wote wenye tabia nzuri kuwa TABIA zao ndio chachu katika MAHUSIANO yao kudumu. Pia msanii Gbros De Voice amesema hivi karibuni ataupload nyimbo hiyo nzuri kwa ajili ya mashabiki na watanzania wote kuipakua( download ) hapa hapa bongoka.com . Zaidi sana ameomba support na kuupokea mziki wake anaoufanya kwani unaelimisha na kuburudisha jamii ya lika zote. Published By www...