Rais John magufuli aagiza walioficha sukari kufichua mara moja  

Rais Dkt. John Magufuli amewataka wafanyabiashara walioficha sukari katika maghala yao, kuanza kuisambaza mara moja
May 06 2016 Rais Magufuli amezungumza na wananchi kwa nyakati tofauti katika mikoa ya Singida na Manyara wakati waliposimamisha msafara wake uliokuwa ukitoka Dodoma kwenda Arusha.
Rais Magufuli ameyazungumza haya matatu na kutoa maagizo kwa wafanyabiashara wanaoficha sukari kuanza kuisambaza mara moja, vinginevyo serikali itachukua hatua kali.
‘Wale wote waliokuwa wameficha sukari waiachie, wasipoiachia sukari, huwezi kuificha kama sindano, nimeshaagiza vyombo vya dola, vikague magodown yote atakayekutwa na sukari ameificha, yule ni mhujumu uchumi kama wahujumu wengine, asije akanilaumu, asijee-akanilaumu, na ninasema kwa dhati’.
‘wewe mfanyabiashara uliyepata nafasi ya Tanzania kuleta bidha za sukari, halafu unanunua unakwenda kuficha ili kusudi wazee hawa wahangaike, ili mwezi mtukufu wa Ramadhani utakapoingia watu wakose sukari, dawa yao ninayo’.  
Akiwa katika miji ya Katesh, Babati, Dareda na Magugu mkoani Manyara Rais Magufuli amepokea malalamiko ya wananchi kuhusu kukosa maeneo kwa ajili ya  shughuli za kilimo na ufugaji na baada ya kupata malalamiko hayo  amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joel Bendera na wakuu wa wilaya za mkoa huo kukamilisha mchakato wa kuyapitia mashamba yote yaliyotelekezwa na wamiliki wake na kuwasilisha taarifa kwake ili afute hati za umiliki wa mashamba hayo na kuamuru wagawiwe wananchi.

Aidha amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Manyara kupanga siku za kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Rais Magufuli amewasili mjini Arusha akitokea Dodoma kwa njia ya barabara na Jumamosi anatarajiwa kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania -JWTZ kundi la 58/15 katika chuo cha mafunzo ya jeshi Monduli.

Comments

Popular posts from this blog

Habari kamili kupatikana kwa Roma