Rais John magufuli aagiza walioficha sukari kufichua mara moja Rais Dkt. John Magufuli amewataka wafanyabiashara walioficha sukari katika maghala yao, kuanza kuisambaza mara moja May 06 2016 Rais Magufuli amezungumza na wananchi kwa nyakati tofauti katika mikoa ya Singida na Manyara wakati waliposimamisha msafara wake uliokuwa ukitoka Dodoma kwenda Arusha. Rais Magufuli ameyazungumza haya matatu na kutoa maagizo kwa wafanyabiashara wanaoficha sukari kuanza kuisambaza mara moja, vinginevyo serikali itachukua hatua kali. ‘Wale wote waliokuwa wameficha sukari waiachie, wasipoiachia sukari, huwezi kuificha kama sindano, nimeshaagiza vyombo vya dola, vikague magodown yote atakayekutwa na sukari ameificha, yule ni mhujumu uchumi kama wahujumu wengine, asije akanilaumu, asijee-akanilaumu, na ninasema kwa dhati’. ‘wewe mfanyabiashara uliyepata nafasi ya Tanzania kuleta bidha za sukari, halafu unanunua unakwenda kuficha ili kusudi wazee hawa wahangaike, ili mwezi ...
Comments
Post a Comment