Posts

Showing posts from 2016
Image
Mchezaji soka wa Cameroon afariki uwanjani 7 Mei 2016 R.I.P Mr Patrick Ekeng Mchezaji wa soka ya kimataifa kutoka Cameroon, Patrick Ekeng, amefariki baada ya kuanguka uwanjani katika ligi ya Romania. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alipoteza fahamu dakika saba tu baada ya kuingia uwanjani kuchukua nafasi ya mchezaji mwingine katika timu yake ya Dinamo Bucharest katika mji mkuu wa taifa hilo, Bucharest. Hakuwa amegusana wala kukaribiana na mchezaji mwingine alipoanguka uwanjani . Matabibu walimkimbiza hospitalini ambako madaktari walijaribu kumfufua kwa zaidi ya saa moja bila kufaulu. Kwa muda wa miaka michache iliyopita wachazaji kadhaa Waafrika wamefariki walipokuwa wakicheza uwanjani.
Image
Rais John magufuli aagiza walioficha sukari kufichua mara moja   Rais Dkt. John Magufuli amewataka wafanyabiashara walioficha sukari katika maghala yao, kuanza kuisambaza mara moja May 06 2016 Rais Magufuli amezungumza na wananchi kwa nyakati tofauti katika mikoa ya Singida na Manyara wakati waliposimamisha msafara wake uliokuwa ukitoka Dodoma kwenda Arusha. Rais Magufuli ameyazungumza haya matatu na kutoa maagizo kwa wafanyabiashara wanaoficha sukari kuanza kuisambaza mara moja, vinginevyo serikali itachukua hatua kali. ‘Wale wote waliokuwa wameficha sukari waiachie, wasipoiachia sukari, huwezi kuificha kama sindano, nimeshaagiza vyombo vya dola, vikague magodown yote  atakayekutwa na sukari ameificha, yule ni mhujumu uchumi kama wahujumu wengine, asije akanilaumu, asijee-akanilaumu, na ninasema kwa dhati’. ‘wewe mfanyabiashara uliyepata nafasi ya Tanzania kuleta bidha za sukari, halafu unanunua unakwenda kuficha ili kusudi wazee hawa wahangaike, ili mwezi ...
Image
GBRO'S DE VOICE AACHIA SINGLE MPYA INAYOTAMBA JIJINI Msanii Gbros de Voice ambae ni chipukizi gumzo kwa watoto na hata watu wazima kwa umahili wake mzuri wa kupangilia sauti na mashahiri, ameongea na bongoka blog juu ya nyimbo yake aliyo isambaza katika media mbalimbali ndani na nje ya nchi kuwa ni nyimbo iliyompa mafanikio mengi katika maisha yake. .Pamoja na kuwa na taalu ma ya UHASIBU aliyoipata kutoka chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) amesema anapendelea sana sanaa ya mziki ikiwa ni kama kipaji alicho nacho kwa lengo la kueli m isha na kuburudisha ja mii. Pia amewahasa wasanii wenzake kutoikwepa elimu kwani inatoa mwangaza  m kubwa katika shughuli zao za kisanii. @ +charles alphonce   Watch Live :    https://www.youtube.com/watch?v=AIOq2oXvaVE Download free music with one click: https://mkito.com/artist/1280789 Watch Live :   https://www.youtube.com/watch?v=AIOq2oXvaVE
Image
Justin Bieber kizimbani Image copyr Image capti Mwanamuziki Justin Bieber ameshtakiwa kwa dola milioni 100,000 kwa madai kwamba alivunja simu. Nyota huyo ametuhumiwa kuivunja simu ya Robert Earl Morgan baada ya kujaribu kumrekodi Bieber wakati alipokuwa akinywa pombeKIsa hicxho kilitokea katika kilabu ya Cle mjini Texas mwezi uliopita. Kulingana na mtandao wa TMZ,Justin Bieber alikasirishwa na kuchukua simu yake na kuivunja. Thamani ya iPhone haifiki dola 100,000. Lakini ameshtakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha kwa sababu simu hiyo ilikuwa na picha ambazo haziwezi kupatikana tena,ikiwemo picha za sherehe ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa bibi yake. Morgan pia anadai kwamba alipoteza idad kubwa ya nambari zake za mawasiliano ya biashara. Image caption Bieber akishikwa koo Bieber bado hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo. Kisa hicho kinaaminika kufanyika jioni ambayo Bieber alionekana kumchoma na sigara Post Malone,ambay amekuwa akimsaidia katika ziara yake ya duniani. P...
Image
Muziki wa Snura - Chura aaa Image caption Snura na albamu yake chura iliopigwa marufuku Tanzania Serikali ya Tanzania imepiga marufuku wimbo na kanda ya video ya muziki kwa jina chura wa msanii Snura Mushi kuchezwa katika vyombo mbalimbali vya habari hadi pale msanii huyo atakapoufanyia marekebisho wimbo huo. Vilevile Serikali imesitisha maonyesho yote ya hadhara ya mwanamuziki huyo hadi pale atakaposajili kazi zake katika baraza la taifa la sanaa BASATA. Hatua hiyo inafuatia maudhui ya utengenezwaji wa video hiyo ambayo serikali inasema inakiuka maadili ya raia wa Tanzania. Serikali imesema kuwa kazi ya mwanamuziki huyo inadhalilisha tasnia ya muziki nchini Tanzania.